Health & Wellness
Mradi wa Mashine ya Kisasa ya Kusagia Nafaka – KIJAEFA
Started February 2026
1 / 7
About This Project
Kikundi cha KIJAEFA, chini ya usimamizi wa Taasisi ya TPAA, kimeanzisha mradi wa kimkakati wa Mashine ya Kusagia Nafaka kwa lengo la kuleta mapinduzi ya kiuchumi katika jamii yetu.
Mradi huu unalenga kutatua changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma bora ya usagaji nafaka kwa gharama nafuu. Kupitia mashine hii, tunazalisha unga safi wa mahindi na lishe, huku tukitengeneza fursa za ajira kwa vijana na wanawake ndani ya kikundi. Huu siyo tu mradi wa biashara, bali ni kitovu cha ujasiriamali kinacholenga kuimarisha usalama wa chakula na kukuza kipato cha mwanachama mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Malengo Yetu ya Baadaye
1. Kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wadogo wadogo.
2. Kutoa elimu ya lishe bora kupitia bidhaa zinazosagwa.
3. Kupanua wigo wa soko la unga wetu nje ya mkoa wetu.
2. Kutoa elimu ya lishe bora kupitia bidhaa zinazosagwa.
3. Kupanua wigo wa soko la unga wetu nje ya mkoa wetu.
Wafadhili waliohusika
Hili mradi huu wa mashine ya kusagia nafaka ukamilike , tulihitaji vifuatavyo: Kwanza , Tulihitaji Mashine/Mitambo yenyewe lakini Pili, Tulihitaji Nyumba au Jengo ambalo mashine hiyo , itawekwa humo.
Hivyo basi, Tulihitaji sana kushikwa mkono na kwa kweli tunawashukuru sana GGML ambao walitupatia Mashine hizi huku Kiwanda cha TPC Moshi DC , wakatujengea nyumba Nzuri kabisa ya kuhifadhi mashine hii.
Hakika Mchango wenu utaendelewa kukumbukwa kwenye mioyo ya wanakikundi na jamii kwa ujumla.

Project Details
- Category
- Health & Wellness
- Start Date
- February 1, 2026
- Status
- Featured Project
Support Our Work
Interested in supporting this project or partnering with KIJAEFA? We'd love to hear from you.
Get In Touch